Tuesday, 15 September 2015

Mchg Paulo Lohay Lucas na Ester Peter

Ni mchg wa kanisa la TAG Temple Revival Ayapara Mbulu

Ibada zetu huanza saa 1.00 asubuhi kila jumapili

Katikati ya wiki ni Jumatano Mafundisho  na Ijumaa maombi saa 10.00 jioni

Karibuni wote kwa ibada za upako

Nina mke mmoja Ester Peter

Nina watoto saba
wanne wa kike na watatu wa kiume

Uchaguzi mkuu Tanzania Octoba 25 - 2015



UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015 Na Mchg Paulo Lukas T.A.G Revival Temple Ayapara

Tudumishe amani tuliyokuwa nayo kwa muda mrefu hapa Tanzania, ambayo ni tunu kutoka kwa Mungu wetu.

Iweje tumwage damu wakati kiongozi asiyekidhi matakwa yetu sisi wana nchi tutamwondoa kwa kura?

Tukubali matokeo ya uchaguzi ambapo yatatokana na kura yako.

Usipopiga kura umepoteza haki yako.

Kumbuka uhuru wetu wa Tanzania ulipatikana bila au pasipo kumwaga damu.

Sisi ni Taifa moja lisilo na udini wala matabaka yoyote. Sisi sote ni ndugu, tunaoana bila kujali kabila.

Asante ni mimi Mchg Paulo Lukas T.A.G Revival Temple Ayapara, Mbulu, Manyara